Moja ya kitu
kinachoudhi kwa mtumiaji wa computer ni pale anapoweka bando lake la wiki au
mwezi ili afanye kazi yake, lakini ghafla anashangaa browser (Google chrome,
Firefox n.k) inaload tu bila kufungua site yoyote. Kama alikuwa
anapakia(upload) au anapakua (download)
file lolote kwenye mtandao linasimama kisa bando
limeisha. Watu wengi wamekuwa wakilalamikia service providers (TigoTanzania, Vodacom, Halotel n.k) japo wakati
mwingine tatizo sio wao. Jambo hili limekuwa likileta mgogoro katika ofisi
mbalimbali. Unakuta boss ametoa kifurushi kwa msaidizi wake kwa ajili ya kazi
fulani. Mara tu msaidizi wa boss anapo-connect internet katika computer ghafla
bando limeisha. Boss anaanza kufoka akimtuhumu msaidizi wake kuwa amelituia
vibaya bando lake. Leo nimekuletea suluhisho la hilo tatizo.
Labda nipende
kukwambia kuwa kitu kinachokula (consume) bando lako kwenye computer yako ni Microsoft
Windows Automatic Update, na Microsoft
Windows Autoamatic Activation (nitaongelea siku ingine hii kitu). Kumbuka
kuwa Windows Operating System (Mfumo endeshi wa windows) na mifumo mingine
endeshi imewekewa “feature” ya “updates” ili kuuweka mfumo endeshi kuwa imara
na kuifanya computer yako kufanya kazi vizuri. Kwa hiyo inashauriwa kuwa
hakikisha Mfumo endeshi(opearating system) unakuwa “updated” ili kuifanya
computer yako kufanya kazi vizuri bila tatizo na kuwa imara (run smoothly and
strong). Lakini sasa update ili ifanyike inahitaji kifurushi cha MB wengine
huita bando kitu ambayo kinahitaji pesa. Sasa kwa hali ya kawaida mfumo endeshi
wa windows imewekewa “Automatic Updates” kuwa kipaumbele cha kwanza (by default) katika vipaumble vya Windows Upadates. Kwa
hiyo ukiunganisha tu mtandao (internet) katika computer yako inaanza kulitumia
bando lako katika ku-update Operating System (OS) bila wewe kujua. Mara tu
kidogo utaona kifurushi chako kimeisha.
Ili kuondokana na hali
hii inatakiwa kuzima automatic updates (disable Automatic Updates), ili bando
lako lisiliwe. Unaweza kuamua kusimamisha kwa muda installation ya Windows Updates mpaka pale utakapoamua wewe-yaani
utapokuwa na bando la kutosha kufanya hivyo. Unaweza kuchelewesha au kuzima Windows Updates
hata kwa siku 35, mwaka mmoja au ukazima moja kwa moja hadi pale utakapofungua
Windows updates. Ili kufanya hivyo basi fuata hatua hapa chini.
[Muhimu: Nimeweka njia nyingi za kuzima
automatic update katika windows10. Kwa hiyo ukiona computer yako haina feature
ya njia mojawapo hapa chini jaribu njia inayofuata]
KUZIMA AUTOMATIC
UPDATES KWA MUDA KWA KUTUMIA SETTING (DISABLING ALL UPDATES)
Kuzima autoamatic
updates kwa muda fuata hatua zifuatazo
1. Bofya window button >> bofya setting
2. Bofya kwenye Update & Security.
3. Bofya kwenye Windows Update.
4. Bofya kwenye button ya Advanced options button.
1. 5. Kwenye
section ya "Pause updates" tumia
Pause until drop-down
menu, na kisha chagua tarehe ya mbele unayotaka automatic update ifanyike kwenye
Windows10.
Utakapomaliza hatua hizi updates itazimwa hadi siku uliyoichagua ifike. Kwa kufanya hivyo utakuwa umefanikiwa kudhibiti bando lako lisipotee bila wewe kuhitaji. Utaweza kumaliza kazi yako kwa bando kidogo sana.
KUZIMA AUTOMATIC
UPDATE KWA MWAKA MMOJA
Kwa nyongeza pia
“Advanced Setting” inakuwezesha kuzima automatic upadate hadi kwa kipindi cha
mwaka mmoja. Fuata hatua hapa chini.
- Fungua Settings.
- Bofya kwenye Update & Security.
- Bofya kwenye Windows Update.
- Bofya kwenye button ya Advanced options
Chini ya section ya "Choose when updates are Installed" tumia orodha ya machaguo, na kisha chagua idadi ya siku ambazo ni 365 ambapo windows itafanya update.
Kitu cha kuzingatia
hapa ni kwamba Option hii haipo kwenye kila computer ya kila mtu. Kwa hiyo kama
computer yako haina feature hii basi endelea na njia nyingine hapa chini mbazo
zitakuwa kweye computer yako.
KUZIMA
AUTOMATIC UPDATES KWA KUTUMIA GROUP POLICY
Kama unatumia Windows 10
Pro, unaweza kutumia Local Group Policy ili kuzima automatic updates moja kwa
moja, au unaweza kubadililisha setting za Windows Update policy ili kuamua lini
updates ziweze kuwa installed
Fuata hatua zifuatazo.
- Fungua Start.
- Andika neno “gpedit.msc” kisha chagua bofya gpedit.msc. Group
Policy Editor itafunguka.
- Nenda kwenye path ifuatayo: Computer Configuration > Administrative Templates > Windows Components > Windows Update
- Bofya mara mbili haraka (double click) “Configure Automatic Updates” policy iliyoko upande wa kulia. Tazama picha hapa chini.
- Chagua (Check) chaguo la Disabled ili kuzima policy
6.Bofya kwenye button ya Apply
7.Bofya kwenye button ya OK
Baada ya kumaliza hatua hizi windows 10 itasimamisha kupakua updates automatic kwenye compuer yako. Ila unaweza kuinstall upadates kwa maamuzi yako kwa kwenda kwenye:
Settings >> Update
& Security >>Windows Update, >> Check for updates
Weka mipaka (limits) ya updates
Kwa njia nyingine,
kama “disabling the policy” haifanyi kazi kwenye computer yako, unaweza kuweka
machaguo ya automatic updates policy kwa kutumia Group Policy Editor ili kuweka
mipaka (limits) ya updates kwenye computer yako.
Fuata hatua hizi:
1. Fungua Start.
2. Kwenye box la kutafuta (search box), andika “gpedit.msc” kasha
bofya
3. Nenda kwenye path ifuatayo:
Computer Configuration >
Administrative Templates > Windows Components > Windows Update
4. Bofya mara mbili ili kufungua Configure
Automatic Updates policy iliyoko upande wa kulia.
5. Chagua chaguo la Enable ili kuiwasha (turn on) policy.
6. Kwenye section ya "Options" chagua chaguo la configure automatic updates kwenye Windows 10: utapata machaguo yafuatyo
2- Notify for download and auto install.
3 - Auto download and notify for install.
4 - Auto download and schedule the install.
5 - Allow local admin to choose setting.
Kisha chagua chaguo 2 - Notify for download and
auto install
7. Bofya button ya Apply
8. Bofya button ya OK
Ukimaliza hatua hizi automatic
updates itazimwa kwenye windows 10. Ila kama kutakuwa na updates mpya za
windows Computer itatoa taarifa (notification) ili uweze kudownload na
kuinstall kwa Kwenda kwenye setting page.
kuzima
automatic updates kwa kutumia Registry
kwenye Windows 10 Pro, unaweza kuzima automatic updates kwa
kutumia Registry. Unaweza kufabya hivyo kwa
kutumia njia mbili tofauti.
Kuzima updates kwa ku-modify Registry
Ili kuzima moja kwa moja kweye Windows 10 modifying the
Registry, use these steps:
Naweka angalizo hapa kuwa kufanya mabadiliko katika
registry ni hatari sana na inaweza uharibifu au matatizo katika windows kama
usipokuwa managlifu. Kwa hiyo nashauri kwamba uhamishe data zako zote (full backup) kabla ya hujaanza na hatua hii.
Fuata hatua zifuatazo ili kuzima updates kwa kutumia registry
1. Fungua Start.
- Kwenye box la kutafuta (search box), andika regedit kasha
bofya regedit ili kuifungua Registry Editor.
3. Nenda kwenye path ifuatayo:
HKEY_LOCAL_MACHINE\SOFTWARE\Policies\Microsoft\Windows
4. Right-click folda la Windows, chagua New, na kisha bofya kwenye chaguo la Key
5. Lipe jina la WindowsUpdate na kisha bofya enter (Name the new key WindowsUpdate and press Enter.)
6 Right-click folda jipya ambalo sasa umelipa jina “WindowsUpdate” chagua new na kisha chagua chaguo la key. (Tazama picha hapa chini)
7. Ipe jina key mpya AU nakisha bofya Enter
8. Right-click kwenye upande wa kulia, chagua New na kisha chaguo la DWORD (32-bit) Value.
9. Ipe jina key mpya NoAutoUpdate n akisha bofya Enter (Name the new key NoAutoUpdate and press Enter)
10. Double-click key mpya uliyotengeneza na badilisha thamani yake kutoka 0 kwenda 1 (Double-click the newly created key and change its value from 0 to 1).
11. Bofya button ya OK.
12. Restart computer yako.
Baada ya kumaliza hizi
hatua, windows updates itaacha kuinstall updates automatic kwenye computer
yako.
Kuweka mipaka ya
updates (Limiting updates) kwa kutumia registry.
Unaweza kutumia
registry kuweka mpango (customize) wa updates ili kuizuia windows ku-updates
automatically
Ili kufanya hivyo
fuata hatua zifuatazo.
1.
1. Fungua Start.
2. Kwenye box la kutafuta
(search box) andika regedit na kisha bofya regedit ili kuifungua.
3. Nenda kwenye path
ifuatayo: HKEY_LOCAL_MACHINE\SOFTWARE\Policies\Microsoft\Windows
4. Right-click folder la Windows kisha
chagua New,kisha bofya chagua la Key(Tazama picha hapa chini)
5. Ipe jina key mpya WindowsUpdate (Name the new key WindowsUpdate and press Enter).
6. Right-click key mpya uliyotengeneza, chagua new, kisha bofya chaguo la key.
7. Ipe jina key mpya AUOptions kisha bofya Enter (Name the new key AUOptions and press Enter).
8. Double click key mpya uliyotengeneza kisha badilisha thani yake kuwa: (Double-click the newly created key and change its value (number only) to:)
Machaguo ya thamani ni
kama nifuatavyo:
2 — Notify for
download and auto install.
3 — Auto download
and notify for install.
4 — Auto download
and schedule the install.
5 — Allow local
admin to choose settings.
Machaguo haya yana
fanya kazi sawa kama kwenye Group Policy settings, na namba 2 ndio chaguo zuri
kwa ajili ya kuzima updates katika windows 10 moja kwa moja.
9. Bofya button ya OK
10. Restart computer yako
Ukimaliza hatua hizi windows 1o itasimamisha
updates zote automayically. Japokuwa utakuwa unapata taarifa (notification)
mara tu baada ya updates mpya kupatikna, Lakini hazita download mpaka utakapoamua
kudownload
Musa Kazimoto
0710100166
No comments:
Post a Comment