KUUNGANISHA MAFILE YA .PDF KATIKA FILE MOJA

 



JINSI YA KUUNGANISHA MAFILE MENGI YA  .pdf  KUWA FILE MOJA



Ili kuunganisha mafaili ya PDF kuwa katika faili moja la PDF fuata hatua zifuazo.

1.    Hakikisha una mafaili ya PDF. Unaweza kupata mafaili hayo kutoka katika Word document, Scanner, FDF creator kutoka katika Cloud Computing n.k (kama unashindwa katika hii hatua basi wasiliana nasi, bofya Contact Us)

2.    Fungua program inayoitwa “Nitro Pro 10”. kama hauna program  bofya HAPA au  pakua Nitro PDF katika bog hii kwa kubofya katika SOFTWARE button hapo juu, au wasiliana nasi 



3.    Bofya Combine click button



4.    Bofya Add Files Button



5.    Chagua sehemu ambapo file lako la PDF lilipo kisha bofya open


6.    File la PFD la kwanza kuwekwa litaonekana hivi



7.    Bofya Add Files button


8.    kisha chagua file jingine halfu bofya open button



9.    File la PDF la pili na la kwanza yataonekna hivi



Unaweza kuendelea na hatua ya 4 hadi ya 6 kutokana na idadi ya mafile uliyonayo

10.   Bofya  create button



11.   Chagua sehemu unayotaka kutunza file lako (mfano desktop), kisha andika jina la file lako (mfano KAVULA COMBINE). Halafu Bofya Save button.



12.    File lako litafunguliwa na software ya Nitro Pro 10 kama unavoona katika picha hapa chini



13.  Bofya file button



14.   Bofya Save As Button



15.   Chagua sehemu unayotaka kutunza file lako. Mfano My Computer > Desktop



16.   Kwenye dialog box itakayokuja chagua sehemu unayotaka kusave file lako. Mfano desktop. kisha andika jina la file lako mfano KAVULA COMBINE



17.   kisha bofya Save Button



18.   Nenda kwenye Desktop, tafuta file lako la KAVULA COMBINE. (Ukiliona basi ujue umefanikiwa)



19.   Ili kulifungua file lako basi utatakiwa kubofya mara mbili kwa haraka (Double Click), kisha file lako lililounganiswa litaonekana kama unavoona hapa chini.



Musa Kazimoto

IT

No comments: