JIFUNZE TEKNOLOJIA YA VIDEO FORMAT KATIKA MIFUMO YA COMPUTER.
Kwa sasa Video Editing imekuwa ni biashara kubwa sana nchini kwetu Tanzania na dunia kwa ujumla. Leo tunashuhudia ongezeko kubwa la ofisi nyingi sana zinazo-shoot video katika maharusi, sendoffs, mihadhara ya siasa, mikutano ya dini, matamasha ya michezo, documentaries na wengine wakiandaa vichekesho na kisha kupost katika mitandao ya kijamii kama vile facebook, youtube, instagram na kwingineko
Kama video editor unapaswa kujua vigezo ambavyo utavitumia ili kuchagua aina ya video format ambayo utaitumia kutokana na hitaji lako. Na hii ni kwa sababu hakuna video format moja ambayo inakubali(fit) kwenye computer zote(computer systems), video platform zote au web browser zote. Na kwa sababu hiyo kuna video format nyingi sana ili kuhakikisha kuwa unachagua video format kutokana na hitaji lako na wapi unataka kutumia video hiyo.
Labda kwa wasiojua video format inamaanisha nini; ni kwamba kila file katika mifumo ya computer lina kitu kinaitwa “file extension” ambayo ndio huitwa file format. Katika Microsoft Word file format ni .txt, .doc, .docs nk. Katika adobe photoshop kuna file extension nyingi sana kama vile .PSD, .EPS, .RAW nk. Katika Filmora9 kuna file extensions zaidi ya kumi kama vile .mkv, .ts, .3gp, .mp4, avi, .mov nk. Na katika Adobe Premier Pro zipo file extension nyingi ikiwa ni pamoja na .mp4, .mov, wmv, avi, avchd, flv, webm nk.
Kwa hiyo unapo-save file lako; mfano kazimoto.mp4, hapo jina la file ni kazimoto na file extension ni .mp4. Kazi ya file extension ni kuonesha kwamba file hilo litafunguliwa kwa mfumo (program) gani. Hivyo basi ukiona file limeandikwa kazimoto.mp4 hapo ujue file hilo litalifunguliwa kwa kutumia video player kama vile VLC Media Player na kama kama file limeandikwa kazimoto.psd basi ujue litafunguliwa kwa kutumia file editor ambayo ni adobe photoshop. (Tazama picha hapo chini). Kwa maana hiyo video format ni aina ya file format ambayo inatumika kutunza file la video la kidijitali katika mifumo ya computer. Video File format hizi zipo nyingi sana na ubora tofauti tofauti kama nikavoeleza hapo chini.
Figure 1: Adobe File Extension (.psd) Nimeona kwenye bandiko langu la leo niweze kushare na wewe video format chache ili ikusaidie pale unapotaka kusave (kutumia) video yako. Maana video editor wengi wamekuwa wakitumia video format wakati mwingine bila kujua na hatima yake anajikuta baadhi ya vitu vinakuwa haviko sawa katika website zao au mitandaoni walikopost. MP4 MP4 ni teknolojia ya mwanzo kabisa ya kusave mafaili ya video. Hii ndio format ambayo vifaa vingi vya kidigitali inasapotiwa. Vifaa vingi vinavyorecodi video hutumia kusave video kwa kutumia hii format bila setting yoyote na hivyo kuifanya formart hii kuwa “Universal Video Format”. Format hii inatoa video kwa ubora wa juu na video yake huwa na size ndogo na hivyo kusababisha watu wengi waipende kuitumia kurushiana kwa Bluetooth, whatsapp na hata kupost instagram n.k. Tatizo la format hii kwamba kuna webbrowser na baadhi ya video players haziwez kusaport video zenye format hii. FLV Vedio format hii inilbuniwa maalumu kwa ajili ya kwajili ya adobe flash media. Hii ndio video format mbayo inasapotiwa na webbrowser zote na video platform zote. Kama wewe unataka kupost video yako ili watu waone video yako katika mtandao; Youtube na Google video basi format hii ndio mahali pake. Hakikisah unaweka video yako kayika format ya .flv (nadhani hapo video editors tunaenda sawa) Faida kubwa ya hii format ni kwamba size yake ni ndogo (MB chache) na hivyo watu itakuwa rahisi kuangalia na kupakua. Tatizo la Format hii ni kuwa haisapotiwi na iOS (simu za Apple) na baadhi ya simu chache. MOV Format hii ilitengenezwa na kampuni ya Apple na waliitengeza maalumu kwa ajili ya Quick Time player. Ila mpaka sasa kuna Matoleo mengi ya Quick Time Player kwa ajili ya Windows ba hivyo kufanya kuifanya MOV kusapotiwa na windows pia. Format hii ina ubora mkubwa ila inachukua nafasi kubwa (MB zake ni kubwa) WMV Format hii ilitengenezwa n akampuni la Microsoft ili wateja wao waweze kucheza au kufungua (play) video zao kwenye windows media player. Na kwenye computer za Apple (Mac OS) unapakuwa WMV player ili kuona video za WMV format. Format hii ina ubora wa hali ya juu ila ina MB kubwa kwa hiyo watu sio rahisi kupakua mtandaoni. AVI Hii ndio video format ya muda mrefu zaidi kuliko zote, ilitengenezwa na Microsoft mnamo mwaka 1992. Pamoja na kuwa ina ubora mzuri sana lakini saizi yake (MB) ni kubwa sana na hivyo kufanya watu kutoangalia wala kupakuwa mtandaoni kwa urahisi. Kwa kipindi hicho watu walikuwa wakishaangalia video zenye format hii wanafuta ili isindelee kujaza hard Disk. AVCHD Kampuni ya Panasonic na sony walitengeneza video format ya AVCHD maalumu kwa ajili ya camera za kidigitali. Kwa hiyo kama unataka kushoot video zenye ubora zaid kwa kutumia camera za kidigitali basi set ya format ya video kuwa AVCHD. Teknolijia ya kupunguza ukubwa wa video bila kuharibu ubora (Video Compression Technology) inayoitwa H.264/MPEG-4 inatumika kupunguza ukubwa wa video zenye format ya AVCHD. Hii imewezesha kuweka file kubwa la video katika CD au DVD yenye uwezo mdogo wa nafasi. Ukiwa makini utagundua kuwa CD nyingi za harusi na sendoff na nyinginezo za kurecord kwa kutumia kamera za dijitali zina file extension ya MPEG ikimaanisha kuwa video hiyo imekuwa compressed. Mwisho. M.Kazimoto IT |
No comments:
Post a Comment