Angalia jibu hapo chini: -
JE UNAHITAJI ANTIVIRUS KWA JILI YA WINDOWS10?
watu wengi wamekuwa wakihangaika na virusi (computer virus) wanaoshambulia document zao katika computer zao. Hivyo mtu aki-install windows
(formart PC), software ya kwanza kuinstall ni kilinzi (Antivurus) ili kuscan
flash disc, external HDD, memory card na kuilinda Operating system na document
zako dhidi ya virus kutoka sehemu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kwenye internet. vilinzi hivyo ni kama vile Comodo Antivirus, Avira Antivirus, Avast Antivirus, Kaspersky Antivirus, Panda Antivirus na nyingine nyingi.
Program hizi zimekuwa zikisababisha watu au taasisi
kuingia gharama kubwa katika kuzinunua.
Taarifa njema ni kwamba kwenye windows10 iko tofauti sana. Hauitaji kabisa antivirus katika Windows10. Microsoft imeweka moja kwa moja ulinzi halali wa computer yako dhidi ya virus (legitimate antivirus protection built into Windows10). Kwa hiyo wala huhitaji kuistall antivirus yingine katika windows10.
Kilinzi cha Windows Defender (Microsoft
Defender Antivirus) katika windows10, mara nyingi hujulikana kama Windows Defender, ni kilinzi (antivirus) ambacho hutoa ulinzi wa kina,
unaoendelea, na wa muda wote dhidi ya hatari za virusi, malware na spyware
kutoka katika barua pepe, apps, clouds na tovuti kwa program au document za computer yako.
Windows Defender hufanya kazi pale ambapo computer
yako iko updated. kwa hiyo hakikisha kwamba muda wote computer yako iko updated.
Kama ni gharama ku-Update basi unaweza ku-update Windows Defender ikawa update
muda wote ili kuilinda computer yako.
Mtandao wa microsoft unaitaja Windows Defender kama Ulinzi wa kizazi kijacho kwenye Windows 10, Windows Server 2016, na Windows Server 2019 ( Next-generation protection in Windows 10, Windows Server 2016, and Windows Server 2019). Bofya Hapa.
Ukitaka
kutumia Windows Defender; bofya start button kisha kwenye serch box andika
Windows Defender, kisha bofya Windows Defender. Itafunguka kama unavoon katika
picha hapo chini.
Hivyo unaweza soma
status ya komputer yako, unaweza ku-update na kuscan pia kama unavyoona katika
picha hapo juu.
Musa Kazimoto.
IT
No comments:
Post a Comment